HITIMANA Thiery,Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa watajipaga kwa ajili ya mechi zijazo baada ya leo kupata sare.
Ikiwa Uwanja wa Uhuru, KMC ilitoshana nguvu ya bila kufungana na Namungo FC leo Aprili 3 2022.
Thiery ambaye alikuwa pia ni kocha wa Namungo FC amesema kuwa hakuwa na chaguo kwa kuwa walipata nafasi lakini wakashindwa kuzitumia.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa kila mechi ni muhimu kushinda ili kupata pointi.
“Tulipata nafasi kwenye mechi yetu ambayo tumecheza ila haikuwa bahati yetu kushinda kutokana na kushindwa kupata matokeo.
“Tumetengeneza nafasi lakini tumeshindwa kuzitumia hivyo kwa mech zijazo tutapambana kupata ushindi kwani muhimu ni kupata pointi,” amesema.
Mchezo uliopita KMC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga.