UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa hauungi mkono kabisa matumizi ya vitochi na badala yake uwezo wa wachezaji pamoja na uwepo wa mashabiki uwanjani ni silaha yao katika kusaka ushindi.
Kesho saa 4:00 usiku Simba ina kibarua ca kusaka ushindi mbele a USGN kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi na ambacho wanakihitaji ni ushindi ili waweze kufuzu hatua ya robo fainali.
Ahmed Ally, Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba amesema:-“Kama Simba SC hatuungi mkono vitendo kama hivyo kwa kuwa sheria zipo kimya kuhusu matumizi ya vitochi lakini kuna timu nyingi zimepeleka malalamiko mengi kuhusu vitochi CAF na kuna mataifa mengi yamelalamika kuhusu vitochi.
“Huo ni utamaduni wa watu wengine inawezekana kwao iliweza kuwapa matokeo lakini Simba huo hauwezi kuwa utamaduni wetu tumeshinda dhidi ya ASEC bila vitochi,tumeshinda dhidi ya RS Berkane bila ya vitochi.
“Hatuna sababu mechi hii ya mwisho kuweza kushinda kwa kutumia vitochi, sisi silaha yetu kubwa kwenye mchezo wetu wa kesho ni kelele za mashabiki wetu, vitochi na masuala mengine yanayohusu mwanga hivyo tuache kwa kuwa sisi ni klabu kubwa barani Afrika,”.
Kikosi cha Simba kimefanya mazoezi kwa ajili ya mchezo wao wa kesho na miongoni mwa nyota ambao wamefanya mazoezi ni pamoja na John Bocco, Bernard Morrison,Mzamiru Yassin na Meddie Kagere.