BUKAYO SAKA ANDOLEWA KAMBI YA TIMU YA TAIFA

BUKAYO Saka ameondolewa katika kikosi cha timu ya Taifa ya England baada ya kukutwa na maambukizi ya Corona.

Saka nyota wa Arsenal alifanya mazoezi na wachezaji wa Timu ya Taifa ya England Jumanne lakini kwa sasa ametengwa St. George Park tangu Jumatano na kwa sasa amerejea nyumbani.

Saka alitweet kuwa ameondolewa katika kikosi cha timu ya Taifa England ila atarudi akipona.

“Nimejisikia vibaya kuweza kuondolewa katika kambi ya Timu ya Taifa ya England lakini nimekutwa na Corona hivyo inanipasa nijitenge mpaka pale nitakapopona.

“Nitakuwa nipo nao hata nikiwa nyumbani wikiendi sitasubiri mpaka kurudi ili kufanya kile ambacho ninakipenda,”.

Kocha Mkuu wa England, Gareth Southgate hataweza kuchagua mbadala wa mshambuliaji huyo ambaye anakuwa ni wa sita ikiwa nk pamoja na Trent Alexander-Arnold, Reece James, Tammy Abraham na Aaron Ramsdale ambaye aliumia Jumatatu.