KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum alikiona cha moto juzi wakati timu yake ikishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya KMC kutokana na kuchezewa faulo za kutosha.
Rekodi zinaonyesha kwamba Fei alichezewa jumla ya faulo 4 zote ilikuwa ni kipindi cha kwanza jambo lililofanya ashindwe kuwa kwenye mwendo ambao alikuwa ameuzoea.
Alikuwa kwenye vita kali na nyota wa KMC Emmanuel Mvuyekule ambaye aliweza kumchezea faulo moja ilikuwa dk ya 21 faulo nyingine Fei alichezewa dk ya 8,10 na 35.
Licha ya kuchezewa faulo naye hakuwa mnyonge kwa kuwa alicheza faulo dakika ya 2 kwa Sadala Lipangile nyota wa KMC na alipiga shuti moja ambalo halikulenga lango ilikuwa dk ya 42.
Mabao kwenye mchezo huo yalifungwa na Adrew Vincent ambaye alijifunga dk 39 katika harakati za kuokoa na Djuma Shaban ambaye alipachika bao dk ya 51.
Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 48 ikiwa nafasi ya kwanza na haijapoteza mchezo.