MORRISON:TUNAFUZU,TUNAJIAMINI

BERNARD Morrison, kiungo wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco amesema kuwa wanaamini kwamba watafuzu hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho.

Kichapo cha mabao 3-0 mbele ya ASEC Mimosas jana Machi 20,2022 kiliyeyusha matumaini ya Simba kutangulia katika hatua ya robo fainali hivyo wana kazi ya kufanya Uwanja wa Mkapa.

“Tunajiamini, tunajiamini na tufafuzu kwa kuwa tumepoteza mchezo hatujatolewa,mchezo wetu ujao ninaamini kwamba tutashinda kila mchezaji atakuwa imara na tutafuzu hatua inayofuata”.

Simba ikiwa na pointi 7 kundi D nafasi ya  3 ina mchezo mmoja mkononi dhidi ya USGN ya Niger yenye pointi 5 nafasi ya 4 unatarajiwa kuchezwa Aprili 3, Uwanja wa Mkapa.

Ili Simba iweze kufuzu hatua ya robo fainali inahitaji ushindi katika mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.