SALAH AINGIA ANGA ZA PSG NA BARCELONA

MOHAMED Salah mshambuliaji wa Liverpool anatajwa kuingia katika rada za PSG na Barcelona ambazo zinahitaji saini yake.

Mkataba wake ndani ya Liverpool kwa sasa una uhai wa miezi 18 na unatarajiwa kumeguka 2023.

Mpaka sasa hakujawa na taarifa yoyote kutoka Liverpool ambao walikaa naye mara ya mwisho Desemva mwaka jana kuhusu kuboresha mkataba wake.

Staa huyo raia wa Misri ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Jurgen Klopp ambage alisistiza kwamba anahitaji huduma ya nyota huyo.