YANGA YASEPA NA POINTI TATU MBELE YA KMC

MSAKO wa pointi tatu umekamilika na ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Yanga 2-0 KMC.
Mabao ya Andrew Vincent aliyejifunga dk 39 na Djuma Shaban dk 51.

KMC walikosa utulivu hali iliyofanya wakose nafasi walizotengeneza na ni kadi 5 za njano wameonyeshwa.
Yanga inafikisha pointi 48.

KMC inakwama kupata pointi mbele ya Yanga msimu huu kwa kuwa ule wa kwanza ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 Uwanja wa Majimaji, Songea.

Yanga haijapoteza mchezo ipo nafasi ya kwanza na pointi 48 baada ya kucheza mechi 18 msimu wa 2021/22.