WATATU WAREJEA YANGA KUIVAA KMC KWA MKAPA KESHO

CEDRICK Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa wanajua kwamba mchezo wao dhidi ya KMC hautakuwa rahisi kesho Uwanja wa Mkapa Jumamosi huku baadhi ya wachezaji wakiwa wameanza kurejea.

Ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 45 inakutana na KMC iliyo nafasi ya 7 na pointi 22 zote zikiwa zimecheza mechi 17.

Kaze amesema:-“Chico ushindi, Farid Mussa na Kibwana Shomari hawa wamerejea na tayari wameanza mazoezi hivyo ni jambo zuri kwetu kuelekea kwenye mchezo dhidi ya KMC.

“Hautakuwa mchezo rahisi kwa kuwa kila timu inahitaji pointi tatu jambo kubwa ni kuona tunaweza kupata ushindi.

“Tunaijua timu ya KMC imekuwa na mwendo mzuri licha ya kwamba ilipoteza kwenye mechi dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo wao uliopita,” amesema.