POCHETTINO KUFUKUZWA PSG KISA KICHAPO MBELE YA REAL MADRID

MAURICIO Pochettino yupo kwenye presha ya kufutwa kazi ndani ya kikosi cha PSG baada ya timu hiyo kutolewa katika mbio za kuwania ubingwa wa UEFA Champions League.

Ni Real Madrid waliweza kuwaondoa katika hatua ya 16 bora kwa jumla ya mabao 3-2 mchezo wao wa pili uliochezwa Uwanja wa Santiago Bernabeu walipoteza kwa kufungwa mabao 3-1.

PSG inatolewa kwa kufungwa jumla ya mabao 3-2 kwa kuwa mchezo wa kwanza PSG ilishinda bao 1-0.

Bao la PSG lilipachikwa kimiani na Kylian Mbappe ilikuwa dakika ya 39 huku yale ya Real Madrid yakipachikwa na Karim Benzema dk 61,76 na 78.

Inaelezwa kuwa Rais wa PSG,Nasser Al-Khelaifi ametoa ripoti baada ya kupoteza mchezo huo jambo linaloonesha kwamba maisha ya Pochettino yamefika mwisho.