WASHAMBULIAJI wawili ambao walikuwa nje kwa muda ndani ya kikosi cha Yanga wamerejea kikosini kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.
Ni Yusuph Athuman ambaye alikuwa nje kwa muda akitibu majeraha ambayo yalikuwa yakimsumbua.
Pia Crispin Ngushi naye pia amerejea kikosini kwa kuwa alikuwa anatibu majeraha pia.
Athuman kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar alipata nafasi ya kucheza lakini Ngushi hakuweza kucheza mchezo huo wakati Yanga ikishinda mabao 3-0 Uwanja wa Mkapa.
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi alisema kuwa uwezo wa wachezaji hao unajulikana na kurejea kwao ni furaha.
“Wachezaji ambao walikuwa nje kwa muda wamerejea na kutafanya tuzidi kuwa imara hivyo tunafurahi kuona wachezaji wanarejea kwenye ubora wao,” amesema.