RALF Rangnick, Kocha Mkuu wa Manchester United amewachana mastaa wa timu hiyo kwa kuwaambia kwamba wanatakiwa kuongeza umakini.
Juzi Manchester United walikosa nafasi nyingi za wazi kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Old Trafford ilikuwa ni Februari 26,2022 na waligawana pointi mojamoja.
Wakiwa wamecheza mechi 6, Uwanja wa Old Trafford ni mabao sita pekee wamefunga United.
Walipiga mashuti 22 na ni matatu yalilenga lango huku wapinzani wao wakipiga jumla ya mashuti 10 na mawili yalilenga lango.
Kocha huyo amesema:”Kazi yetu ni kusaidia timu kutengeneza nafasi za kutosha na kuweza kuzitumia.
“Kama tungekuwa na nafasi mbili au tatu dhidi ya Watford tungejiuliza kwa nini, lakini nafasi nyingi tulizokuwa nazo zilitosha kabisa kutupa ushindi, tunahitaji kuongeza makali mbele ya lango, ukikosa nafasi nyingi kiasi hicho ni ngumu kushinda,”.