MUDA WA KUJIBU MASWALI YA MZUNGUKO WA KWANZA KWA VITENDO

    NI kitu gani ambacho wachezaji mlishindwa kukifanya kwenye mzunguko wa kwanza katika kusaka ushindi kwenye mechi ambazo mlikuwa mnacheza?

    Ni jambo gani ambalo benchi la ufundi mlikwama kulifanya kwenye mechi ambazo mlikuwa mnaziongoza na mwisho mkapata matokeo ambayo hayakuwa kwenye mpango wenu.

    Ilikuaje mashabiki mkwakwama kushangilia kwenye mechi ambazo mliweza kufika uwanjani mwanzo mwisho na badala yake mkawa mnazomea ama mkawa tofauti na wengine baada ya mchezo?

    Waamuzi ilikuaje katika kutimiza zile sheria 17 ambazo mmekabidhiwa na kuzisoma kwa ukamilifu na mwisho ikawa ni adhabu?

    Kwa nini wachezaji waliweza kufungiwa kwenye mechi kadhaa kutokana na makosa ambayo waliyafanya kabla ama baada ya dakika 90 kukamilika uwanjani?

    Bado kuna wachezaji ni mwendo wa ngumi jiwe uwanjani kwa kizazi cha sasa? Hapana yale yote yaliyopita mzunguko wa kwanza lazima maswali yapatikane kwa vitendo mzunguko wa pili.

    Ipo wazi kwamba kila mmoja ana swali lake ambalo linamuhusu kuanzia kwa wachezaji, benchi la ufundi, waamuzi, mashabiki mpaka wadau.

    Muhimu ni kuona kwamba yale maswali ambayo yanajibika basi na yapewe majibu maalumu kwa vitendo.

    Kwa mfano kama ni mchezaji alishindwa kucheza kwa kujituma ama alikosa nafasi ambazo alizipata kufunga basi yale maelekezo ambayo alipewa mzunguko wa kwanza anapaswa kuyafuata.

    Ikiwa kuna wachezaji ambao ni pasua kichwa kwa mzunguko wa kwanza basi yale yote wayaweke kando na sasa waje na mpango mpya kwa mzunguko wa pili.

    Tunajua kwamba wapo wachezaji ambao wanahesabu mpya kwa mzunguko wa pili hilo ni muhimu kuweza kulitimiza kwa kufanya kazi bila kuchoka.

    Ukweli ni kwamba uwezo wa kushinda kwa wachezaji upo hivyo wanachotakiwa kufanya ni kutimiza majukumu yao bila ya kuchoka pale ambapo wanapata nafasi.

    Mashabiki wanastahili pongezi kwa kuwa wapo pamoja na timu muda wote hivyo kwa wakati huu ni mwendelezo wa burudani bila kuchoka kwa kushangilia timu zao.

    Kujitokeza uwanjani ni jambo moja na kushangilia bila kuchoka ni jambo la pili na hilo limekuwa likiwa likiwapa nguvu wachezaji kufanya kazi yao kwa umakini pia.

    Benchi la ufundi yale makosa ambayo yalitokea mzunguko wa kwanza ni muda wake kuweza kuyafanyia kazi kwa kuwa hakutakuwa na mwingine wa kucheza kwa msimu huu wa 2021/22.

    Wachezaji pia hili liwe kwenye mpango kazi kwamba wanakwenda kukamilisha ile ngwe ya mwisho ambayo itakuwa wazi kwa kila mmoja baada ya mechi kukamilika.

    Hakuna ushindi ambao unaweza kupatikana ikiwa hakutakuwa na maandalizi hivyo hilo ni muhimu kufanyika kwa umakini mkubwa.

    Wale ambao hawakuwa kwenye mwendo mzuri mzunguko wa kwanza huu ni muda wa hesabu na kufanyia kazi makossa ambayo waliyafanya katika mzunguko ule ambao umekamilika.

    @dizo_click

    Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU
    Next articleSIMBA KURUDI KUJIPANGA UPYA KUWAKABILI BERKANE