MKONGWE wa Arsenal, Paul Merson, amesisitiza klabu hiyo inatakiwa kufanya haraka kuwaongezea mikataba nyota wa kikosi hicho, Bukayo Saka na Emile Smith Rowe.
Kwa msimu huu wa 2021/22 Saka na Smith Rowe wamekuwa chachu ya mafanikio ndani ya Arsenal chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta.
Merson amesema nyota hao wamekuwa muhimu ndani ya kikosi hicho msimu huu kutokana na mchango wa kusaka matokeo chanya uwanjani.
Mkataba wa Saka unatarajiwa kufika ukingoni 2024 na Smith Rowe mkataba wake ni mpaka 2026 unatarajiwa kumeguka.
“Arsenal ina wachezaji wazuri wawili spesho ambao wanafanya timu kuwa bora, Bukayo na Emile hawa itapendeza wakipewa mikataba ya muda mrefu hata kila mmoja akipewa miaka mitano sio mbaya,” amesema Merson.