SIMBA:TUTARUDI NA MABEGI YA POINTI BONGO

MTENDAJI Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa wanaamini kwamba watarudi na mabegi ya pointi mgongoni baada ya kukamilisha mchezo wa leo Februari 27 dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Simba ni vinara wa kundi D kwenye Kombe la Shirikisho wakiwa na pointi nne kibindoni wakiwa wamecheza mechi mbili, walishinda mbele ya ASEC Mimosas mabao 3-1 kisha wakalazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya USGN ya Niger.

Leo inatarajiwa kumenyana na RS Berkane ya Morocco ambayo imetoka kupoteza mchezo wake uliopita dhidi ya ASEC Mimosas hivyo unatarajiwa kuwa mchezo mgumu kwa timu zote.

Barbara amesema:”Tupo imara kwa ajili ya mashindano haya ya kimataifa na kikubwa ni kuomab Watanzania waweze kutuombea, ambacho tunaamini ni kwamba tutarudi Jumatatu na mabegi ya pointi.

“Baada ya kumaliza kazi ya kusaka pointi mbele ya USGN Niger tulishukuru Mung una benchi la ufundi kuna vitu limeona tuna amini kwamba watafanyia kazi na tunahitaji kushinda,” amesema.