LIGI ya Mabingwa Ulaya inaendelea kuwasha moto na kesho Februari 23 mchezo kati ya Atletico Madrid v Manchester United unasubiriwa kwa shauku kubwa.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Wanda Metropolitan na ni wa hatua ya 16 bora ndani ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Swali kubwa ni kuhusu Cristiano Ronaldo na rekodi zake ambazo ameweka na kwa sasa yupo ndani ya Manchester United.
Ronaldo amekuwa na rekodi bora mbele ya Atletico Madrid akiwatungua mara 25 katika mechi 35.
Staa huyi kipindi alipokuwa ndani ya Real Madrid alipata nafasi ya kucheza zaidi na Atletico Madrid na alicheza nao mara mbili fainali ilikuwa ni 2014 na 2016.
Atletico Madrid na Man United zitakutana kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.