KOCHA Antonio Conte amedai kuwa sera ya usajili ya Tottenham inadhoofisha kikosi, huku akiweka wazi kuwa wachezaji waliowasajili wakati wa dirisha la Januari wamekwenda kukivuruga zaidi kikosi chao badala ya kukiboresha.
Muitaliano huyo amedai kuwa timu yake sasa ina nafasi ya asilimia moja tu kumaliza top 4 katika Premier, Tottenham
Katika usajili wa Januari, Spurs waliwaongeza viungo Dejan Kulusevski na Rodrigo Bentancur kutoka Juventus, huku Tanguy Ndombele, Bryan Gil, Dele Alli na Giovani Lo Celso wakiondoka “Badala ya kukiboresha kikosi, tumekidhoofisha,” alisema.
“Bentancur na Kulusevski ni wazuri kwa Tottenham siku zijazo, kwa sababu Tottenham wanatafuta wachezaji makinda, wanaweza kukua na kuendelea, siyo wachezaji walio tayari. Hili ni tatizo. Nimegundua sasa kwamba haya ndiyo maono ya klabu.”