|
UKURASA unaendelea kufunguliwa hasa katika anga za kimataifa ilikuwa ni baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas leo kwa mara nyingine tena kuna jambo litatokea baada ya dakika 90.
Leo ni leo, wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa, Simba wanatarajiwa kusaka pointi tatu mbele ya USGN ya Niger na tayari kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco kipo tayari.
Muda mfupi kabla ya wachezaji wa Simba kukwea pipa kuelekea Niger,Spoti Xtra iliweza kufanya mazungumzo na Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally ambaye aliweza kuweka wazi hesabu za timu hiyo kimataifa namna hii:-
“Tupo vizuri na msafara wetu umejumuisha wachezaji 23 hawa wanakwenda kutimiza majukumu kwa ajili ya kusaka ushindi.
“Chris Mugalu,Kibu Dennis na Hassan Dilunga hawa bado ni majeruhi na Mzamiru Yassin na Rally Bwalya hawa wameondoka kikosini wana matatizo ya kifamilia.
Ratiba kimataifa ipoje?
“Tuna ratiba ngumu nay a kazi ambayo tunakwenda kuifanya tukianza na USGN Februari 20 kisha tutakuwa na mchezo dhidi ya RS Berkane ya Morroco Februari 27 hapo unaona namna gani ratiba itakuwa ngumu.
“Lakini ukweli ni kwamba hatuna mashaka kuhusu ratiba yetu kwani tupo na wachezaji wenye ubora na kila mmoja anajua majukumu yake ndio maana tumeondoka na wachezaji wengi.
“Siku 10 ambazo tutazitumia huku tunapeperusha bendera ya Tanzania na hatuna mashaka kwenye mechi zetu.
Kwa nini Chama licha ya kwamba hatacheza?
“Tunajua kwamban Chama hatacheza lakini ni mchezaji muhimu kwetu na siku ambazo tutakaa ni nyingi tyungesema abaki hapa Tanzania kuna vitu vingepungua kwake ikiwa ni pamnoja na ile kasi ambayo ameanza nayo pamoja na ule muunganiko ulioanza kuonekana ndani ya timu.
“Kumbuka kwamba tukimaliza kazi kimataifa kwa mechi zetu hizi mbili tunarudi tena kucheza mechi za ligi sasa kama angebaki ina maana tungerudi kuanza naye upya hivyo hizi ni sababu za kiufundi.
“Mchezo wetu kwenye ligi unaofuata utakuwa dhidi ya Biashara United hivyo wapinzani wetu wana kazi ya kuweza kujiaandaa vizuri kwani hatuna jambo dogo itakuwa ni mwendo wa dozi katika mechi ambazo tutacheza.
“Nazungumza na timu zote na sio 15 sio vinara wa ligi pekee hapana timu zote zinapaswa kujiaandaa kwa sababu tukitoka huko kwenye mashiundano ya kimataifa ile dozi ya CAF itahamia kwenye mechi za NBC.
Ugenini ni pointi ngapi malengo?
“Pointi moja kupata ugenini sio jambo baya ila kwanza ni pointi tatu ili kwenye mechi mbili tuweze kupata pointi sita ikisdhindikana sana tunahitaji pointi mbili kwenye mechi za ugenini.
“RS Berkane hatuna mashaka nao kwa kuwa tayari benchi la ufundi limeshawasoma wapinzani na kujua ni aina gani ya mbinu zitafaa. Najua utasema kwamba kuhusu Tuisila Kisinda hilo halitupi hofu kumbuka kwamba alikuwepo hivi karibuni na tuliweza kutwaa ubingwa na yeye akiwa yupo hapa Tanzania.
“Kwa timu ambazo zinabaki Tanzania kwa siku hizi 10 ambazo tutakuwa ugenini wao wasijisahau, wasianzane kuzurura wafanye mazoezi kwa kuwa tukirudi ni mwendo wa dozi tu wasisahau kwamba tumetoka kushinda mbele ya Ruvu Shooting mabao mengi tu ambayo ni 7-0 hivyo wasijisahau tunakwenda na tutarudi.
“Mashabiki tunajua kwamba wanapenda kuja Morocco lakini haiwezekani wao tunaomba dua zao ziwe pamoja nasi kwa kuwa dua inafika sehemu yoyote ile ni wakati wetu kuendelea kuwa na furaha,” alimaliza Ally.
|
|