KIUNGO Deus Kaseke katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Biashara United alitumia dakika 8 akitokea benchi na alichukua nafasi ya Feisal Salum.
Alipiga pasi 9 na alicheza faulo moja wakati Yanga ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Biashara United
Yanga imetinga hatua ya robo fainali inaungana na Azam FC iliyowatungua Baga Friends timu ngumu kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit mabao 6-0.
Pia timu nyingine ambayo imetinga hatua ya robo fainali ni Polisi Tanzania iliyoshinda mbele ya Tanzania Prisons katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine.