KYLIAN Mbappe staa wa Klabu ya PSG aliweza kuwatungua bao la ushindi Real Madrid katika mchezo wa UEFA Champions League hatua ya 16 bora.
Ilikuwa dakika ya 90+4 nyota huyo aliweza kupachika bao hilo katika mchezo huo wa kwanza uliokuwa mkali mwanzo mwisho.
PSG katika Uwanja wa Parc des Princes waliweza kupiga jumla ya mashuti 21 na katika hayo ni mashuti 8 pekee yalilenga lango la Real Madrid.
Madrid wao walipiga mashuti matatu pekee na hakuna ambalo lililenga lango ndani ya dakika 90 za mchezo huo.
Ni kona 7 PSG walipiga huku Madrid wao wakipiga kona moja pekee huku umiliki wa mpira kwa PSG ikiwa ni asilimia 58 na 42 kwa Real Madrid.