MANCHESTER CITY YAPIGA MKONO HUKO

PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City usiku wa kuamkia leo ameshuhudia vijana wake wakisepa na ushindi mnono katika mchezo wa raundi ya 16, UEFA Champions League.

Timu hiyo ambayo inaongoza Ligi Kuu England iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Sporting katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Jose Alvalade.

Ni mabao ya Riyad Mahrez dakika ya 7,Bernardo Silva alitupia mawili dakika ya 17 na 44, Phil Foden alitupia moja dk ya 32 na Raheem Steling alitupia moja dakika ya 58.

Katika mchezo huo City ilipiga jumla ya mashuti 15 na ni sita yalilenga lango huku Sporting wao wakipiga mashuti matatu na hakuna hata moja ambalo lililenga lango.