WAPINZANI WA SIMBA WAPIGA MATIZI YA MWISHO MKAPA

WAPINZANI wa Simba, ASEC Mimosas leo Februari 12,2022 wamefanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Mkapa.

Ni kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kesho Februari 13, Uwanja wa Mkapa dhidi ya Simba.

Utakuwa mchezo wa kwanza kwa timu hizo ndani ya kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika ambapo kila timu hesabu zake ni kusepa na pointi tatu.

Nahodha wa ASEC Mimosas, Cisse Abdul Karim amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo na kila timu inahitaji ushindi na tunawaheshimu wapinzani wetu,”.