KIUNGO wa Simba, Bernard Morrison kwa msimu wa 2021/22 ndani ya kikosi cha Simba ameyeyusha dakika 500 katika mechi za Ligi Kuu Bara.
Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 15 ambazo ni dakika 1,350 alikosekana katika dakika 850 uwanjani.
Kabla ya kusimamishwa kutokana na kile kilichoelezwa kwamba ni utovu wa nidhamu mechi yake ya mwisho ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba na Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Katika msimamo ipo nafasi ya pili na pointi zake kibindoni ni 31 na imetupia mabao 16 huku Morrison akiwa hajafunga hata bao moja.
Kiungo huyo amehusika katika mabao matatu ambapo moja alisababisha penalti mbele ya Polisi Tanzania na ilifungwa na Rally Bwalya na alitoa pasi mbili za mabao zote kwa mapigo huru ilikuwa mbele ya Ruvu Shooting kwa pigo la kona ilifungwa na Meddie Kagere na ya pili ilikuwa ni pigo la faulo lilifungwa na Mzamiru Yassin.