SENEGAL ni mabingwa wa AFCON 2021 kwa ushindi wa penalti 4-2 baada ya dakika 120 kukamilika bila kufungana dhidi ya Misri kwenye bonge moja ya fainali.
Mshindi alipatikana kwa mikwaju ya penalti ambapo ni Senegal walianza kupiga kupitia kwa Coulibary ambaye kufunga penalti hiyo ya kwanza.
Coulibary alifunga penalti ya kwanza kwa Senegal na Zizou alipiga penalti ya kwanza kwa Misri iliyokuwa na Mohamed Salah na ilizama nyavuni mazima.
Ikumbukwe kwamba kipindi cha kwanza Sadio Mane aliweza kukosa penalti baada ya kipa wa Misri kuweza kuikoa penalti hiyo.
Kabla ya kupiga penalti hiyo kipindi cha kwanza Salah alionekana akimpa maelekezo kipa wake kwa namna ya upigaji wa Mane ambaye alikosa penalti hiyo
Miamba hao wawili wanajuana kwa kuwa wanacheza pamoja ndani ya kikosi cha Liverpool kinachoshiriki Ligi Kuu England.
Ni yeye Mane alifunga penalti ya mwisho ya ushindi iliyowafanya Senegal kutanagzwa kuwa mabingwa wapya kwa Afcon ya 2021 iliyofanyika nchini Cameroon ambao wao ni washindi watatu.