AUBA:TATIZO NI ARTETA

PIERRE Emerick Aubameyang amethibitisha kwamba Kocha Mkuu, Mikel Arteta ndiyo sababu ya yeye kuondoka ndani ya Arsenal ambao wataendelea kumlipa pauni 230,000 kwa wiki hadi msimu huu.

Auba alitangazwa kuwa mchezaji mpya wa Barcelona juzi baada ya kukamilisha usajili wake akiwa huru.

Kabla ya kuvunja mkataba wake uliomuweka huru, Arsenal ilikubaliana naye kumlipa pauni milioni 7 kwa awamu.

Barca itahusika na mshahara wake wote kuanzia msimu ujao lakini kwa sasa itamlipa pauni 100,000 kila wiki huku Arsenal ikimlipa pauni 230,000.

Auba amesema:”Nadhani tatizo lilikuwa kwake tu, (Arteta) na alifanya maamuzi siwezi kusema zaidi. Hakuwa na furaha nitabaki mtulivu sana na hivyo ndivyo ilivyo,”.