SIMBA YASHINDA KWA PENALTI MBELE YA PRISONS

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba leo wepata ushindi mbele ya Tanzania Prisons baada ya mechi tatu za ugenini kushindwa kupata matokeo.

Bao la ushindi limepachikwa na Meddie Kagere baada ya mwamuzi wa kati kuamua ipigwe penalti ambayo ilikuwa ikionekana kupingwa  na wachezaji wa Prisons.

Jumla Simba inakuwa imefunga mabao 15 katika mechi 14 za ligi na leo ni Chris Mugalu aliweza kupiga shuti lililolenga lango.

Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa makosa wameyaona na watayafanyia kazi.

“Makosa tumeyaona na tutayafanyia kazi kwa ajili ya mechi zetu zijazo,”.

Linakuwa ni bao la tano la Kagere ndani ya ligi msimu wa 2021/22.