TPLB Yamteua Yahaya Abushehe Kuwa Kaimu Ofisa Habari Mpya

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemtangaza rasmi Yahaya Abushehe kuwa Kaimu Ofisa Habari wa bodi hiyo, akichukua nafasi ya Karim Boimanda ambaye atapangiwa majukumu mengine ndani ya taasisi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 14, 2026 na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Cornel Barnabas, uteuzi huo ni sehemu ya mabadiliko ya kiutendaji katika Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha bodi hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi wa Abushehe unaanza kufanya kazi mara moja, ikiwa ni hatua ya kuimarisha zaidi utendaji wa kitengo hicho muhimu katika uendeshaji wa Ligi Kuu Tanzania.