MARA baada yakupoteza mchezo wa kwanza ndani ya NBC Premier League, uongozi wa Yanga SC umebainisha kuwa ulijua kuwa siku moja watapoteza mchezo.
Mei 13, 2026 ubao wa Uwanja wa Airtel, Singida ulisoma Dodoma Jiji FC 3-2 Yanga SC ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa mabingwa watetezi kupoteza ndani ya ligi msimu wa 2025/26.
Timu hiyo Mei 6, 2026 ilimfuta kazi Pedro Goncalves mara baada ya ubao wa Uwanja wa KMC Complex kusoma KMC FC 0-1 Yanga SC.
Kwa sasa timu inanolewa na Kocha Mkuu, Ahmid Moallin na Patrick Mabed amba watakuwa na kikosi kwenye mechi 7 zilizobaki ndani ya ligi.
Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC amesema walikuwa wanatambua watafungwa kwa kuwa ni sehemu ya matokeo ndani ya uwanja.
“Tulijua ipo siku moja tutafungwa kwa kuwa huu ni mpira na haya yote ni matokeo. Imetokea jana dhidi ya Dodoma Jiji FC tumepoteza lakini bado tunaongoza ligi tukiwa na faida ya tofauti ya pointi na mechi mkononi.Mashabiki ni muda wa kuendelea kushikamana kwa sasa kwani bado tuna nafasi ya kutwaa ubingwa,”.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.