Kule Uturuki kunatarajiwa kupamba moto ambapo timu nne bado zinapambana kupata nafasi ya kwenda kucheza mechi ya Fainali ya Europa League. Je nani na nani kuingia Fainali?
Mbilinge mbilinge zitakuwa kwenye mechi hii ya Aston Villa dhidi ya Nottingham Forest kutoka kule Uingereza hawa wote wanajuana vyema kabisa. Hii ni mechi ambayo ni ya kisasi kwa mwenyeji baada ya kupoteza mechi ya kwanza ugenini kwa bao 1-0.
Hii ni mechi ya lazima kwa vijana wa Unai kushinda baada ya kupoteza mechi yao iliyopita kule ugenini huku Forest wakicheza kwa utulivu zaidi wakiwa na faida ya matokeo ya awali lakini ni mechi ambayo Villa wanahitaji zaidi wapate matokeo ili wacheze fainali baada ya muda mrefu.
Aston Villa wao wanaingia uwanjani wakiwa na lengo kubwa kushambulia ili waweze kusawzisha goli mapema kabisa, lakini kwa upande wa Nottingham Forest wao wanaweza kutumia mbinu ya kujilinda zaidi kutokana an mtaji wa bao moja ambalo wanalo lakini kushambulia kunaweza kukawa kwa mbali.
Tengeneza mkwanja kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Si mara ya kwanza kukutana ukizingatia hawa wawili wanashiriki ligi moja yaani EPL. Lakini huku ni kwenye michuano ya Europa kila timu inaweza ikapata matokeo mbele ya mwenzake ukiachilia nafasi zao walizopo kwenye msimamo wa ligi kuu.
Nafasi kubwa ya kushinda mechi hii wanapewa vijana wa Unai kutokana na kiwango bora ambacho wamekionesha msimu huu, lakini pia uwepo wa kocha wao ambaye haya ndiyo mashindano yake, kwani amewahi kufanya vizuri akiwa na Sevilla ya kule Hispania.
Villa wana ubora wa kikosi na uwezo wa kushambulia kwa nguvu, lakini Forest wana faida ya utulivu na mpangilio wa kujilinda pamoja na mashambulizi ya kushitukiza.
Matokeo yatategemea nani atakuwa na ufanisi zaidi katika dakika za mwanzo. Villa wakifunga mapema watafungua mechi, lakini Forest wakistahimili au kufunga kwanza, basi wataweza kudhibiti mwelekeo wa mechi na kufunga njia ya Villa kurejea.
Kule Ujerumani nako Freiburg atamleta kwake Braga ambao walishinda mechi yao ya kwanza ya Nusu Fainali kule Ureno hivyo leo hii ni kisasi kwa mwenyeji pia. Jisajili hapa.
Braga anaingia uwanjani akiwa na faida ya bao 1, baada ya kushinda mechi ya kwanza kwa mabao 2-1 huku weenyeji wao wakiutazama mchezo huu kama wa kufa na kupona kwani hakuna kitu ambacho kitaswasaidi zaidi ya kufunga magoli mengi pekee.
Kule Ureno, Braga ni moja ya timu ambazo zinafanya vyema kule Ureno wakiwa nafasi ya 4 mpaka sasa kwenye msimamo wa ligi. Huku kwa upande wa wenyeji wao pale Bundesliga wanashikilia nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi huku wakiwa na takwimu mbaya za mechi 3 za mwisho wakiwa wamepoteza.
Hii ni mechi ya maamuzi kwa pande zote mbili huku leo hii ushindi unaweza ukaamuliwa kwa pande zote mbili hasa kama timu ina washambuliaji wazuri kwani kwenye hatua hizi magoli ndio kitu muhimu sana kuliko chochote.
Kwa upande wa Freiburg wao wana mfumo na uthabiti, wakati Braga wana kasi na hatari ya moja kwa moja. Timu itakayoweza kulazimisha mpinzani wake kucheza kwa mtindo usio wake itakuwa na nafasi kubwa ya kushinda.
Kwa ujumla ni kwamba, Freiburg watajaribu kugeuza mchezo kuwa wa polepole na wenye udhibiti, huku Braga wakitaka kuufanya uwe wa kasi na wa wazi. Nani atafanikiwa kulazimisha mtindo wake, huyo ndiye atakayekuwa na nusu ya ushindi.