Nusu Fainali Yamoto Rayo Vallecano Kuminyana Vikali Strasbourg

Leo Alhamisi tarehe 30 Aprili saa 22:00 Uwanja wa Estadio de Vallecas utakuwa jukwaa la pambano la hatua ya nusu fainali ya Conference League kati ya Rayo Vallecano na Strasbourg.

Mechi hii ni ya kihistoria kwa timu zote mbili, kwani zote zimefika hatua hii kwa mara ya kwanza katika historia yao. Rayo, wanaotoka kitongoji cha wafanyakazi Madrid, wanatafuta kuendeleza safari yao ya ajabu baada ya mafanikio makubwa nyumbani, huku Strasbourg wakilenga kulinda rekodi yao nzuri katika mashindano haya.

Rayo Vallecano wanaingia kwenye mechi wakiwa na rekodi nzuri sana katika Uwanja wa Vallecas, wakiwa hawajafungwa katika mechi 5 kati ya 6 za nyumbani kwenye mashindano ya Ulaya. Katika hatua ya robo fainali, walinusurika kwa nyuzi baada ya ushindi wa 3-0 ugenini kugeuka na kuwapokea bao la kuwaondoa watani wa Ugiriki AEK Athens, wakifuzu kwa jumla ya mabao 4-3.

Strasbourg kwa upande wao walionyesha nguvu za kushambulia baada ya kufungwa 2-0 ugenini na Mainz, kabla ya kuwafunga 4-0 nyumbani na kugeuza mkondo. Timu ya Ufaransa ilimaliza hatua ya makundi ikiwa ni bingwa kwenye msimamo wao.

Rayo Vallecano wanajulikana kwa mtindo wao wa kushambulia kwa kasi na ukali wa hali ya juu, huku winga wao Alvaro Garcia na Jorge De Frutos wakiwa na mabao 12 kila mmoja msimu huu. Kocha Iñigo Pérez, ambaye ana miaka 38 tu, ameleta utulivu wa ulinzi huku akidumisha falsafa ya ushambuliaji.

Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Strasbourg, chini ya kocha Gary O’Neil (aliyechukua nafasi ya Liam Rosenior aliyekwenda Chelsea), wameendelea kucheza kwa nguvu na kujiamini. Wao pia wana rekodi nzuri ya kutofungwa ikiwa imefikia mechi 11 kati ya 12 za mashindano. Strasbourg wana silaha muhimu nyuma, akiwemo beki wa zamani wa Chelsea Ben Chilwell aliye na uzoefu wa kushinda Ligi ya Mabingwa.

Timu zote mbili zina changamoto za wachezaji kabla ya mechi hii. Rayo Vallecano watawakosa Randy Nteka na Luiz Felipe kutokana na majeruhi. Walikosa beki wao mkuu Florian Lejeune kwenye mechi za mwisho za ligi kutokana na adhabu, lakini anatarajiwa kurejea kwa ajili ya pambano hili muhimu.

Mabingwa wakutoa Odds kubwa tayari washazitoa, Vuna maokoto yako sasa

Strasbourg wana majeruhi wengi zaidi yakiwemo Mathis Amougou, Valentín Barco, Guéla Doué, Aaron Anselmino, na mshambuliaji Joaquín Panichelli ambaye anaumia kwa msimu mzima. Hii itakuwa pigo kubwa kwa kina cha kikosi chao, hasa safu ya ulinzi. Mojawapo ya faida kubwa ya Rayo ni uwanja wao wa nyumbani. Vallecas ni uwanja mdogo wenye uwezo wa kuchukua takriban mashabiki 15,000, lakini ni ngome mwiba kwa timu kubwa huko Uhispania. Barcelona, Real Madrid, na Atlético Madrid wameshindwa kushinda Vallecas msimu huu.

Katika mechi ya hivi karibuni dhidi ya Real Sociedad, Rayo walionyesha moyo wa kipekee waliingizwa mkwara 1-3 katika dakika za mwisho, lakini wakafunga mabao mawili ya kuokoa sare hadi dakika ya 90+9. Jisajili

Kwa kuzingatia hali zote, timu inayopendelewa kidogo ni Rayo Vallecano kutokana na rekodi yao ya nyumbani na ari ya kikosi. Strasbourg wana ubora ubora wa kiungo, lakini wamepoteza wachezaji wengi muhimu kutokana na majeruhi. Rayo wana motisha ya kufika fainali kwa mara ya kwanza kwenye klabu yao ya umaskini ya La Liga.