AUBAMEYANG HUYO BARCELONA BURE

ARSENAL imekubali kumuacha nyota wake Pierre Aubameyang ajiunge na Barcelona bure ili aweze kupata changamoto mpya wakati mwingine akisepa ndani ya Ligi Kuu England.

Auba mwenye miaka 32 anaondoka ndani ya kikosi hicho ikiwa ni muda mfupi baada ya kuvuliwa kitambaa cha unahodha.

Mshambuliaji huyo hakuweza kucheza katika timu hiyo tangu Desemba 6 2021.

Anasepa ndani ya Arsenal akiwa amecheza mechi 163 na ametupia mabao 92 anaondoka ndani ya Arsenal inayotumia Uwanja wa Emirates baada ya kuvunja mkataba wake ambao ulikuwa umesalia miezi 18.