MEDDIE Kagere mshambuliaji namba moja kwa kutupia ndani ya Simba kwa msimu wa 2021/22 ndani ya ligi akiwa ametupia mabao manne na pasi moja ameyeyusha dakika 414 bila kufunga.
Novemba 19,2021 ilikuwa Uwanja wa CCM Kirumba na Simba iliweza kushinda mabao 3-1 na kusepa na pointi tatu mazima.
Leo, Kagere anatimiza siku ya 74 bila kufunga bao wala kutoa pasi kwenye mechi za ligi na Simba kwenye msimamo ipo nafasi ya pili,ikitupia mabao 14 kibindoni.
Mbele ya Geita Gold aliyeyusha dakika 36,mbele ya Yanga dakika 80,KMC alitumia dakika 90,Azam FC dakika 65,Mbeya City dakika 21, Mtibwa Sugar dk 90 na mbele ya Kagera Sugar alitumia dakika 32.
Kwenye mechi hizo 7 za ligi jumla Kagere alitumia dakika 414 bila kufunga wala kutoa pasi ya bao na aliweza kushuhuda timu hiyo dakika 270 mfululizo ikicheza kwenye mechi za ugenini bila kufunga.