Mechi atakazokosekana Diarra Yanga SC 2025/26

BAADA ya kuwa kwenye adhabu ya kufungiwa mechi 3 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) kutokana na makosa ya kinidhamu mlinda mlango namba moja wa Yanga SC, Djigui Diarra tayari ameshakosekana kwenye mchezo mmoja wakiwa nyumbani na langoni alianza Aboutwalib Mshery.

Yanga SC 3-0 Tanzania Prisons, Aprili 4,2026. Mchezo huu Yanga SC walikuwa nyumbani, Uwanja wa KMC Complex. Mzunguko wa kwanza alianza Diarra ugenini waliposhinda kwa goli 1-0.

Kituo kinachofuata ni Pamba Jiji FC vs Yanga SC, Aprili 8,2026. Wananchi watakuwa ugenini. Mchezo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Yanga SC vs TMA Stars mchezo wa CRDB Federation Cup ambapo Yanga SC watakuwa nyumbani huu utakuwa ni mchezo wa tatu kwa Diarra kukosekana.

Baada ya hapo adhabu yake itakuwa imegota mwisho atarejea uwanjani kutimiza majukumu yake kwenye mechi za ushindani.

Mchezo wa Yanga SC vs Mbeya City, Aprili 16,2026. Mabingwa watetezi watakuwa nyumbani. Uwanja wa KMC Complex huu huenda akarejea katika kazi.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.