Zesco United Yasimamishwa Kushiriki Ligi Kuu Zambia

Klabu ya Zesco United FC imesimamishwa kushiriki katika Ligi Kuu ya Zambia, baada ya klabu hiyo kupeleka mgogoro unaohusiana na masuala ya soka katika Mahakama za kawaida, jambo ambalo linakiuka kanuni za uendeshaji wa soka zinazotaka migogoro ya aina hiyo kushughulikiwa ndani ya vyombo vya soka pekee.

Kutokana na kusimamishwa huko, mechi zote za ligi zilizopangwa kuchezwa na Zesco United zimesitishwa hadi pale suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi rasmi.

Hata hivyo, klabu hiyo ina nafasi ya kukata rufaa kupinga uamuzi huo huku ikisubiri hatma ya ushiriki wake katika ligi hiyo.