Yanga SC vs Tanzania Prisons, Aprili 4, 2026 ni mchezo unaofuata katika ratiba ya NBC Premier League kwa vinara 2025/26.
Baada ya mapumziko ya FIFA ni mzunguko wa 18 unaendelea katika ligi namba nne kwa ubora Afrika.
Saa 12:30 Yanga SC watakuwa Uwanja wa KMC Complex kuwakabili Tanzania Prisons kutoka Mbeya katika msako wa pointi 3 muhimu.
Ikumbukwe kwamba mchezo wa mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ulisoma Tanzania Prisons 0-1 Yanga SC, goli la ushindi likifungwa na Depu ambaye alianzia benchi.
Depu ndani ya ligi amefunga magoli 6 katika hayo mawili alifunga kwa penati tayari amerejea kwenye uwanja wa mazoezi baada ya kuwa chini ya madaktari.
Yanga SC inaendelea na mazoezi kambini Avic Town Kigamboni na miongoni mwa wachezaji waliopo kambini ni Aboutwalib Mshery, Maxi Nzengeli, Pacome, Boka, Kibwana Shomari na Allen Okelo.
Yanga SC inaongoza ligi ikiwa na pointi 38 baada ya mechi 16 inakutana na Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 15 na pointi 13.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.