KIUNGO wa Azam FC, Feisal Salum ni namba moja kwa mastaa waliohusika katika magoli mengi ndani ya NBC Premier League 2025/26.
Ni mabao 11 amehusika katika kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Florent Ibenge ndani ya ligi namba 6 kwa ubora.
Fei amefunga jumla ya magoli 6 na ametoa pasi 5. Azam FC baada ya mechi 15 safu ya ushambuliaji imefunga jumka ya magoli 21.
Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya 3 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 29 vinara ni Yanga SC wenye pointi 38.
Fabrice Ngoy wa Namungo FC ni namba mbili akiwa amehusika katika magoli 8 kati ya 14 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya 8 msimamo wa ligi na pointi 21 baada ya mechi 17 yeye amefunga tu mpaka akiwa ni namba moja kwa mastaa wenye magoli mengi.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.