Yanga Soccer School na EMWANI waja na mashindano bab kubwa

Yanga SC na Kampuni ya EMWANI wameandaa mashindano yatakayofanyika 28/03/2026 kituo cha TFF Kigamboni.

 Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari amesema huo ni muitikio wa Watanzania katika mradi Yanga Soccer School na mshindi wa kwanza atapata milioni 3, mshindi wa pili milioni moja na watakaoishia nusu faiinali watapata laki 5.

“Mradi wetu wa Yanga Soccer School umekuwa kwa kiasi kikubwa kama ambavyo Pitso Mosimane alitutabiria. Kijana Mendez amejitokeza kuunga mkono jitihada kupitia mashindano kwa akademi,”.

“Mshindi wa mashindano ya Yanga SC na EMWANI atapata kiasi cha Tsh 3m, mshindi wa pili atapewa milioni 1, watakaoishia nusu fainali watapata 500,000. Zawadi hizi ni udhamini wa EMWANI hivyo wadau mbalimbali ambao wanamilki vitu vya akademi wanahimizwa kufanya usajili mapema jangwani au kupitia email ya Yanga. Washiriki wanapaswa kuwa chini ya miaka 18.

“Klabu ya Yanga inatangaza rasmi vituo mbalimbali ambavyo vina akademi wanakaribishwa. Usahili umeanza pale Jangwani. EMWANI watachagua wachezaji kumi ambayo watawadhamini kujiunga na Yanga Soccer School,” amesema Kamwe.