Katika eneo la kutengeneza pasi za mwisho ndani ya NBC Premier League wakali wawili wapo kwenye chati wakiwa wametengeneza pasi nyingi ambazo ni 5.
Ni Ellie Mpanzu wa Simba SC yupo sawa na kiungo wa Azam FC Feisal Salum ambao hawa wote wamekuwa katika ubora kwenye eneo la kutengeneza pasi za mwisho.
Wengine kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) ni Duke Abuya wa Yanga SC na Ibrahim Imoro wa Singida Black Stars kila mmoja akiwa ametengeneza pasi 4 za magoli.
Beki Israel Mwenda na kiungo Maxi Nzengeli wa Yanga SC hawa wote wawili wametengeneza pasi.
Andrew Chamunu wa Namungo FC, Larmin Jarjou wa Singida Black Stars na Baraka Maranyingi wa Mbeya City hawa wametoa pasi 3.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.