Kuelekea kwenye mchezo wa NBC Premier League, Mtibwa Sugar vs Yanga SC, Uwanja wa Jamhuri Dodoma, benchi la ufundi la wageni limebainisha kuwa linapitia kwenye kipindi kigumu cha ratiba.
Pedro Goncalves, Kocha Mkuu wa Yanga SC amebainisha kuwa wamekuwa kwenye mechi ngumu za ushindani na wanapitia katika ratiba ngumu wakati huu wa mfungo wa Ramadhan kwa baadhi ya wachezaji.
Katika mchezo uliopita ugenini baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ulisoma TRA United 0-0 Yanga SC wakigawana pointi mojamoja.
Pedro amesema: “Maandalizi yetu kuelekea mchezo wa kesho yamekuwa na changamoto kubwa. Tulitoka Arusha jana baada ya safari ndefu na tulipowasili hapa, wachezaji wengi walifanya mazoezi ya kurejesha nguvu (recovery), huku wengine wakifanya mazoezi mepesi uwanjani.
“Kwa kipindi cha wiki tatu hadi nne zilizopita tumekuwa na ratiba ngumu. Mchezo wa kesho utakuwa wa saba ndani ya siku 21 jambo ambalo ni changamoto kubwa. Pia tunapaswa kuzingatia kuwa baadhi ya wachezaji wako kwenye mfungo wa Ramadhani pamoja na safari za mara kwa mara kwa ujumla tunapitia kipindi kigumu sana cha msimu,”.
Yanga SC kwenye msimamo ni namba moja ikiwa na pointi 37 baada ya mechi 15 inatarajiwa kumenyana na Mtibwa Sugar iliyo nafasi 9 na pointi 21 baada ya mechi 16.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.