Singida Black Stars vs Simba SC ni mchezo unaofuata kwenye ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa wababe hawa wawili.
Jumatano ya wiki hii wababe hawa wanatarajiwa kukutana Uwanja wa Airtel kwenye msako wa pointi tatu muhimu.
Singida Black Stars mchezo wake uliopita kwenye ligi ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Yanga SC wakiwa nyumbani.
Wanawakaribisha Simba SC kwenye mchezo mwingine wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Machi 11,2026.
Simba SC kwenye msimamo ipo nafasi ya 4 ikiwa na pointi 24 kibindoni inakutana na Singida Black Stars nafasi ya 9 ikiwa na pointi 19.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.