Meridianbet Yachochea Mapinduzi ya Usafi Kinondoni kwa Msaada wa Mapipa ya Taka

Katika hatua ya kuunga mkono juhudi za kulinda mazingira na afya za wananchi, Meridianbet imetoa mapipa ya taka katika maeneo ya umma kwa Kata mbalimbali za wilaya ya Kinondoni. Msaada huu unalenga kuimarisha usimamizi wa taka, kupunguza uchafuzi wa mazingira, na kuhamasisha utamaduni wa usafi katika maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu kila siku.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Afisa Mawasiliano wa Meridianbet, Nancy Ingram aliwasifu wafanyakazi wa usafi kwa mchango wao mkubwa kwa jamii. “Hawa ni mashujaa wa afya ya jamii yetu. Kazi yao ni ngumu lakini ya muhimu sana. Kama Meridianbet, tunatambua mchango wao mkubwa na tumeona ni vyema kuonyesha kuthamini kazi yao kwa kuwapatia vifaa vya msingi vya kujikinga na mazingira hatarishi wanapokuwa kazini,” alisema.

Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi, Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Manispaa ya Kinondoni aliipongeza Meridianbet kwa hatua hiyo, akieleza kuwa ni mfano bora wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na Serikali. Alibainisha kuwa msaada huo utarahisisha kazi ya ukusanyaji taka na kuimarisha mazingira ya kazi kwa watumishi wa usafi, huku ukiwapa wananchi mazingira safi na salama zaidi.

Mpango huu ni sehemu ya mkakati mpana wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) unaotekelezwa na Meridianbet nchini. Kupitia miradi ya kijamii, kampuni imekuwa ikiwekeza katika sekta za elimu, afya, michezo na ustawi wa vijana, ikiweka mbele dhamira ya kuleta maendeleo endelevu yanayogusa maisha ya Watanzania moja kwa moja.

Kwa kuendelea kushiriki katika miradi ya kijamii yenye tija, Meridianbet inaimarisha nafasi yake si tu kama kiongozi wa burudani ya michezo ya kubahatisha, bali pia kama mdau muhimu wa maendeleo ya jamii. Msaada huu wa mapipa ya taka ni ushahidi wa vitendo kwamba maendeleo ya kweli huanzia katika mazingira safi na jamii yenye kujali ustawi wa kila mmoja.