Al-Ittihad Yapiga Bao Kubwa Sokoni, Lorch na Aziz Ki Watua Rasmi Libya

Klabu ya Al Ittihad ya Libya imetangaza rasmi usajili wa wachezaji wake wapya, ikionyesha dhamira ya kuimarisha kikosi katika kipindi hikic ha dirisha dogo ili kufikia lengo la kufanya vizuri mwishoni mwa msimu huu.

Miongoni mwa nyota wa waliotambulishwa ni Thembinkosi Lorch (Afrika Kusini) ambaye atavaa jezi namba 11, namba yenye heshima na historia kubwa ndani ya klabu hiyo.

Wakati huohuo, kiungo mshambuliaji kutoka Burkina Faso Stéphane Aziz Ki atavaa jezi namba 32.

Hii ni taarifa kubwa inayoambatana na matarajio kutoka kwa mashabiki na wadau wa Al Ittihad.

Ni nyakati za kusisimua kwa klabu hiyo yenye mafanikio nchini Libya, inapojiandaa kwa changamoto na kufikia malengo yake msimu huu.

Thembinkosi Lorch (Afrika Kusini) – Sh3.8 bilioni (kutoka Wydad Casablanca)

Adem Alilet (Algeria) – Sh1.26 bilioni (kutoka USM Alger)

Stéphane Aziz Ki (Burkina Faso) –Sh952 milioni (kutoka Wydad Casablanca)

Onuche Ogbelu (Nigeria) – Ametoka Espérance Sportive de Tunis (Thamani haijawekwa wazi)

Ahmad Benali (Libya) – Ametoka Virtus Entella (thamani haijawekwa wazi)

Anatole Abang (Cameroon) – Ametoka Al-Bataeh Club (Thamani haijawekwa wazi)