Yanga SC vs JS Kabylie, Jumapili ya kazi kwa wawakilishi wa Tanzania kutupa karata ya mwisho katika anga la kimataifa.
Mchezo huo ni muhimu kwa Yanga SC kupambania malengo yakutinga hatua ya robo fainali wakiwa nafasi ya tatu na pointi 5 huku wanaowania nafasi hiyo wengine ni AS Far Rabat hawa wapo nafasi ya pili na pointi 8.
Yanga SC anahitaji ushindi wa angalau magoli 2 bila kuruhu huku akisubiri matokeo ya mpinzani wake AS Far Rabat ambaye atakuwa kazini dhidi ya Al Ahly ambao wameshakata tiketi kutinga hatua ya robo fainali CAF Champions League.
Far Rabat yeye anahitaji sare ama ushindi pekee kujihakikishia nafasi yakutinga hatua ya robo fainali ikitokea akapoteza basi afungwe kuanzia magoli 2 hapo atampa nafasi Yanga SC kuonga hatua iayofuata lakini itategemea matokeo ya Wananchi kwenye mchezo wa Jumapili.
JS Kabylie kwenye msimamo wa kundi B hawana chakupoteza kwa kuwa wapo nafasi ya 4 na pointi 3 ushindi hautamuondoa alipo atabaki hapohapo.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.