Azam FC vs AS Maniema, Jumamosi New Amaan Complex

Azam FC vs AS Maniema, Jumamosi New Amaan Complex ni mchezo ujao kwa wawakilishi wa Tanzania katika anga la kimataifa.

Ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi kwenye msako wa kutinga hatua ya robo fainali.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza Azam FC ilipoteza dhidi ya AS Maniema hivyo itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu zakupoteza mchezo wa ugenini.

Katika msimamo wa kundi B, Azam FC ipo nafasi ya tatu imekusanya pointi 6 baada ya mechi 4 huku nafasi ya nne ikiwa mikononi mwa Nairobi United.

AS Maniema ipo nafasi ya pili kwenye msimamo imekusanya jumla ya pointi 9 sawa na vinara Wydad Casablanca wote wakiwa wamecheza jumla ya mechi 4 msimu wa 2025/26.

Uongozi wa Azam FC umewaita mashabiki kwa wingi kujitokeza Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar saa 1:00 usiku kuwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.