Mshahara wa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, umeongezeka kila mwaka hadi Dola za Kimarekani Milioni 6.1 (takriban Shilingi bilioni 15 za Tanzania) kutoka Dola Milioni 1.4 mwaka 2016 wakati wa Sepp Blatter.
Haya ni baadhi ya matokeo ya utafiti uliofanywa na Gazeti la ‘Le Monde’ unaofichua muundo wa Mshahara wa mwaka wa Rais wa FIFA tangu aingie madarakani.
Mnamo Februari 26, 2016, Gianni Infantino kutoka Italia alichaguliwa kuongoza FIFA, akichukua nafasi ya Sepp Blatter, ambaye alishukiwa kwa tuhuma za rushwa.
Blatter alikuwa analipwa Dola Milioni 1.4 (takriban TZS 3.5 bilioni) kila mwaka. Hata hivyo, mabadiliko ambayo Infantino alileta kwenye soka yamesababisha ongezeko la mshahara pamoja na bonasi.
Katika kipindi cha miaka 10 tangu Muitaliano huyo awe Rais wa FIFA, amekuwa mmoja wa watu tajiri zaidi duniani.