Klabu ya Yanga inadaiwa kufikia makubaliano na klabu ya Radomiak Radom ya Poland katika uhamisho wa mshambuliaji Laurindo Dilson Maria Aurélio “Depu”, raia wa Angola, ambaye anatarajiwa kutua rasmi mitaa ya Jangwani.
Depu anasajiliwa kuchukua nafasi ya Andy Boyeli, ambaye amerejea katika klabu yake, huku Yanga ikilenga kuimarisha eneo la ushambuliaji kuelekea michezo ijayo ya ndani na kimataifa.
Kwa ujio wa Depu, sasa Yanga itakuwa na safu ya washambuliaji watatu wenye ushindani mkubwa wakiwemo Prince Dube, Clement Mzize pamoja na Depu, hali inayotarajiwa kuongeza nguvu na mbadala katika safu ya mbele ya kikosi hicho.
Usajili huo unaonekana kuwa sehemu ya mkakati wa Yanga kujiimarisha zaidi katika mbio za mataji, huku mashabiki wakisubiri kuona mchango wa mshambuliaji huyo mpya uwanjani.