Meneja wa zamani wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjær ameonesha nia ya kurejea klabuni hapo kama kocha mkuu wa muda mpaka mwisho wa msimu baada ya kufutwa kazi kwa Ruben Amorim.
Menejimenti ya klabu hiyo imedokezwa kuhusu mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu hiyo kuwa tayari kuchukua mikoba ya kukinoa kikosi hicho bila kujali ukomo wa mkataba wake klabuni hapo.
Man United inafanya tathimini ya majina ya makocha wanaowania nafasi hiyo kwa muda huku ikiangazia kumteua kocha wa kudumu mwishoni mwa msimu wa 2025/26. Kwa wiki timu hiyo ipo chini ya Daren Fletcher kama kocha wa mpito.