Camara ni njano na kijani

Mohamed Damaro Camara rasmi ni mali ya Yanga SC ikiwa ni zawadi kwa mashabiki ndani ya 2025 kwa kazi ndani ya 2026.

Desemba 31,2025 Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wamemtambulisha rasmi Camara kuwa ingizo jipya kwenye kikosi hicho kinachotetea ubingwa.

Hayo yote ni baada ya makubaliano kwa pande zote mbili kuhusu kupata huduma yake na makubaliano yamefika mpaka mchezaji kutangazwa.

Bado Yanga SC wapo sokoni wakiendelea kusaka wachezaji wapya kuelekea msimu mpya unaendelea wa 2025/26.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.