Mchambuzi wa soka nchini, Hans Rafael, ametoa taarifa kupitia mitandao ya kijamii akidai kuwa uongozi wa Simba SC umejadili mpango wa kuachana kabisa na kocha Suleiman Matola, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kumpokea kocha mkuu mpya.
Kwa mujibu wa Hans Rafael, uongozi wa klabu hiyo umeweka mezani wazo la kutoa nafasi kwa kocha mpya kuunda benchi lake lote la ufundi bila mipaka yoyote, ikiwa ni mkakati wa kuboresha utendaji na matokeo ya timu.
Ujumbe wa Hans Rafael
Hans aliposti ujumbe ufuatao:
“JUST IN: Uongozi wa Simba umejadili mpango wa kuachana mazima na kocha Seleman Matola, ili kumpa uhuru wa kufanya kazi kocha mkuu ajae. Simba wanataka kocha mkuu aje na wasaidizi wake full.”
Ujumbe huo umeibua mjadala mpana miongoni mwa mashabiki wa Simba na wadau wa soka, hususan kutokana na nafasi muhimu ambayo Matola ameicheza katika benchi la ufundi la klabu hiyo kwa misimu kadhaa.