Mashetani Wekundu, Manchester United, wamelazimika kugawana pointi baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya West Ham United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa katika dimba la Old Trafford.
United walianza kupata bao dakika ya 58 kupitia kwa Diogo Dalot, baada ya shambulizi lililoanzia upande wa kulia na kumaliziwa kwa ustadi na beki huyo.
Hata hivyo, West Ham hawakukubali kupoteza mchezo na walirejea mchezoni dakika ya 83 kupitia kwa Magassa, aliyefunga baada ya mpira wa faulo uliosababisha msongamano kwenye eneo la hatari la United.
Matokeo hayo yanaifanya Man United kuendelea kupoteza nafasi muhimu ya kupanda kwenye msimamo wa ligi, huku West Ham wakiondoka na pointi muhimu ugenini.