Wababe wa Kariakoo Kuwasha Moto Ligi Kuu – Simba na Yanga Dimboni Leo

LIGI Kuu ya kabumbu Tanzania bara inaendelea tena leo Desemba 4, 2025 kwa michezo miwili ambapo wababe wa Kariakoo, Simba Sc na Young Africans watashuka dimbani kwenye viwanja tofauti kuzisaka alama tatu.

Katika dimba la KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam Wananchi, Yanga Sc watakuwa wenyeji wa Fountain Gate Fc majira ya saa 10:00 jioni wakati Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc wakiwa wenyeji wa Mbeya City katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni saa 1:00 usiku.

16:00 Yanga Sc vs Fountain Gate Fc
🏟️ KMC Complex, Mwenge

19:00 Simba Sc vs Mbeya City Fc
🏟️ Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni

MSIMAMO
1. JKT TZ — mechi 10 — pointi 17
2. Pamba Jiji — mechi 8 — pointi 15
3. Mashujaa — mechi 9 — pointi 13
4. Namungo — mechi 8 — pointi 12
5. 𝗬𝗮𝗻𝗴𝗮 𝗦𝗰 — 𝗺𝗲𝗰𝗵𝗶 𝟰 — 𝗽𝗼𝗶𝗻𝘁𝗶 𝟭𝟬
6. Mtibwa — mechi 8 — pointi 10
7. Fountain — mechi 9 — pointi 10
8. 𝙎𝙞𝙢𝙗𝙖 𝙎𝙘 — 𝗺𝗲𝗰𝗵𝗶 𝟯 — 𝗽𝗼𝗶𝗻𝘁𝗶 𝟵